Native Bible

Genesis 22:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”

Genesis 22:1 in English

Genesis 22:1 · Berean Standard Bible

Some time later God tested Abraham and said to him, “Abraham!” “Here I am,” he answered.

Context

1Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.” 2Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” 3Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.