Mwanzo 17:18
Genesis 17:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”
Genesis 17:18 in English
Genesis 17:18 · Berean Standard Bible
And Abraham said to God, “O that Ishmael might live under Your blessing!”
Context
16Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.” 17Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 18Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!” 19Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki.* Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. 20Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.