Native Bible

Genesis 15:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake.

Genesis 15:12 in English

Genesis 15:12 · Berean Standard Bible

As the sun was setting, Abram fell into a deep sleep, and suddenly great terror and darkness overwhelmed him.

Context

10Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. 11Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza. 12Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. 13Kisha Bwana akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. 14Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.