Wagalatia 6:16
Galatians 6:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Amani na rehema viwe na wote wanaofuata kanuni hii, na juu ya Israeli wa Mungu.
Galatians 6:16 in English
Galatians 6:16 · Berean Standard Bible
Peace and mercy to all who walk by this rule, even to the Israel of God.
Context
14Mungu apishie mbali nisije nikajivunia kitu chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu. 15Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu! 16Amani na rehema viwe na wote wanaofuata kanuni hii, na juu ya Israeli wa Mungu. 17Hatimaye, tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, kwa maana nachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu. 18Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.