Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

talanta 100* za fedha, ngano kori 100,* divai bathi 100,* mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote.

Ezra 7:22 in English

Ezra 7:22 · Berean Standard Bible

up to a hundred talents of silver,* a hundred cors of wheat,* a hundred baths of wine,* a hundred baths of olive oil,* and salt without limit.

Context

20Kitu kingine chochote kinachohitajika kwa ajili ya Hekalu la Mungu wenu ambacho unatakiwa kukitoa, waweza kukitoa kutoka hazina ya mfalme. 21Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ngʼambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu, 22talanta 100* za fedha, ngano kori 100,* divai bathi 100,* mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote. 23Chochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe? 24Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.