Native Bible

Ezekiel 44:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba.

Ezekiel 44:26 in English

Ezekiel 44:26 · Berean Standard Bible

and after he is cleansed, he must count off seven days for himself.

Context

24“ ‘Katika magombano yoyote, makuhani watatumika kama mahakimu na kuamua hilo jambo kufuatana na sheria zangu. Watazishika sheria zangu na maagizo yangu katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa, nao watatakasa Sabato zangu. 25“ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti, lakini, kama mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hajaolewa, basi aweza kujitia unajisi kwa hao. 26Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba. 27Siku atakapoingia katika ukumbi wa ndani wa mahali patakatifu ili kuhudumu, atatoa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe, asema Bwana Mwenyezi. 28“ ‘Mimi nitakuwa ndio urithi pekee walio nao makuhani katika Israeli. Msiwape wao milki, mimi nitakuwa milki yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.