Ezekieli 42:5
Ezekiel 42:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia* ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo.
Ezekiel 42:5 in English
Ezekiel 42:5 · Berean Standard Bible
Now the upper chambers were smaller because the galleries took more space from the chambers on the lower and middle floors of the building.
Context
3Mbele ya zile dhiraa ishirini za ule ua wa ndani unaoelekeana na ile njia ya ua wa nje, kuliinuka vyumba virefu kimoja baada ya kingine vya ghorofa tatu. 4Mbele ya hivi vyumba kulikuwa na njia ya ndani yenye upana wa dhiraa kumi na urefu wa dhiraa mia moja. Milango yake ilikuwa upande wa kaskazini. 5Basi vyumba vya juu vilikuwa vyembamba zaidi, kwa kuwa ujia* ulichukua nafasi zaidi ndani yake kuliko katika vyumba vya sakafu ya chini na vya katikati ya jengo. 6Vyumba katika ghorofa ya tatu havikuwa na nguzo, kama kumbi zilivyokuwa nazo, kwa hiyo eneo la sakafu ya vyumba vya juu lilikuwa ni dogo kuliko la sakafu ya chini na ya kati. 7Kulikuwa na ukuta wa nje uliokuwa sambamba na vile vyumba na ukumbi wa nje, ulitokeza urefu wa dhiraa hamsini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.