Ezekieli 42:11
Ezekiel 42:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini,
Ezekiel 42:11 in English
Ezekiel 42:11 · Berean Standard Bible
with a passageway in front of them, just like the chambers that were on the north. They had the same length and width, with similar exits and dimensions.
Context
9Vyumba vya chini vilikuwa na ingilio upande wa mashariki unapoingia kutoka ukumbi wa nje. 10Upande wa kusini kufuata urefu wa ukuta wa ukumbi wa nje, unaopakana na ukumbi wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje, kulikuwa na vyumba 11vyenye ujia unayopita mbele yake. Hivi vilifanana na vile vyumba vya upande wa kaskazini, vilikuwa na urefu na upana ulio sawa, mahali pa kutokea na vipimo vyake vilikuwa sawa. Kama ilivyokuwa milango ya upande wa kaskazini, 12ndivyo ilivyokuwa milango ya vyumba vya upande wa kusini. Kulikuwa na ingilio kuanzia mwanzo wa njia ambao ulikuwa sambamba na ukuta wa pili uliokuwa upande wa mashariki, ambako ndiko kwa kuingia vyumbani. 13Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia Bwana watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.