Ezekieli 40:19
Ezekiel 40:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia moja* upande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini.
Ezekiel 40:19 in English
Ezekiel 40:19 · Berean Standard Bible
Then he measured the distance from the front of the lower gateway to the outside of the inner court; it was a hundred cubits * on the east side as well as on the north.
Context
17Kisha akanileta katika ukumbi wa nje. Huko nikaona vyumba vingine pamoja na njia iliyokuwa imejengwa kuzunguka ukumbi wote, kulikuwa na vyumba thelathini vimepangana kando ya hiyo njia. 18Njia hii iliyojengwa iliambaa na lango, ikiwa na urefu sawa na lango, hii ilikuwa ni njia ya chini. 19Kisha akapima umbali kutoka ndani ya lango la chini mpaka nje ya ukumbi wa ndani, nao ulikuwa dhiraa mia moja* upande wa mashariki na dhiraa mia moja upande wa kaskazini. 20Kisha akapima urefu na upana wa lango linaloelekea kaskazini, kukabili ukumbi wa nje. 21Vyumba vyake vilikuwa vitatu kila upande, kuta zilizogawanya vyumba na baraza ilikuwa na vipimo sawa na zile kuta za lango la kwanza. Zilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.