Native Bible

Ezekiel 39:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka nchi za adui zao, mimi nitajionyesha kuwa mtakatifu kwa kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi.

Ezekiel 39:27 in English

Ezekiel 39:27 · Berean Standard Bible

When I bring them back from the peoples and gather them out of the lands of their enemies, I will show My holiness in them in the sight of many nations.

Context

25“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu. 26Wataisahau aibu yao na jinsi walivyoonyesha kutokuwa waaminifu kwangu mimi wakati waliishi salama katika nchi yao, bila kuwa na mtu yeyote wa kuwatia hofu. 27Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka nchi za adui zao, mimi nitajionyesha kuwa mtakatifu kwa kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi. 28Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma. 29Sitawaficha tena uso wangu, kwa maana nitamimina Roho wangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana Mwenyezi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.