Ezekieli 33:3
Ezekiel 33:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu,
Ezekiel 33:3 in English
Ezekiel 33:3 · Berean Standard Bible
and he sees the sword coming against that land and blows the ram’s horn to warn the people.
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao, 3naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu, 4kama mtu yeyote asikiapo sauti ya tarumbeta hakukubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. 5Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angelijiokoa mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.