Ezekieli 29:2
Ezekiel 29:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote.
Ezekiel 29:2 in English
Ezekiel 29:2 · Berean Standard Bible
“Son of man, set your face against Pharaoh king of Egypt and prophesy against him and against all Egypt.
Context
1Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote. 3Nena, nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri,
joka kubwa ulalaye katikati ya vijito vyako.
Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe;
niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.” 4Lakini nitatia ndoana katika mataya yako
nami nitawafanya samaki wa vijito vyako
washikamane na magamba yako.
Nitakutoa katikati ya vijito vyako,
pamoja na samaki wote
walioshikamana na magamba yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.