Native Bible

Ezekiel 20:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani.

Ezekiel 20:10 in English

Ezekiel 20:10 · Berean Standard Bible

So I brought them out of the land of Egypt and led them into the wilderness.

Context

8“ ‘Lakini waliniasi na hawakunisikiliza, hawakuondolea mbali sanamu za machukizo ambazo walikuwa wamezikazia macho, wala kuondolea mbali sanamu za Misri. Ndipo nikasema, nitawamwagia ghadhabu yangu na kutimiza hasira yangu dhidi yao huko Misri. 9Lakini kwa ajili ya Jina langu nilifanya kile ambacho kingelifanya lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa waliyoishi miongoni mwao na ambao machoni pao nilikuwa nimejifunua kwa Waisraeli kwa kuwatoa katika nchi ya Misri. 10Kwa hiyo nikawaongoza watoke Misri na kuwaleta jangwani. 11Nikawapa amri zangu na kuwajulisha sheria zangu, kwa kuwa mtu anayezitii ataishi kwa hizo. 12Pia niliwapa Sabato zangu kama ishara kati yangu nao, ili wapate kujua kuwa Mimi Bwana niliwafanya kuwa watakatifu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.