Native Bible

Ezekiel 11:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Watairudia nchi na kuondoa vinyago vyote vya upotovu na sanamu zote za machukizo.

Ezekiel 11:18 in English

Ezekiel 11:18 · Berean Standard Bible

When they return to it, they will remove all its detestable things and all its abominations.

Context

16“Kwa hiyo sema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ingawa niliwapeleka mbali miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, lakini kwa kitambo kidogo mimi nimekuwa mahali patakatifu kwao katika nchi walizokwenda.’ 17“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitawakusanyeni kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’ 18“Watairudia nchi na kuondoa vinyago vyote vya upotovu na sanamu zote za machukizo. 19Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. 20Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.