Ezekieli 10:13
Ezekiel 10:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.”
Ezekiel 10:13 in English
Ezekiel 10:13 · Berean Standard Bible
I heard the wheels being called “the whirling wheels.”
Context
11Yalipozunguka, yalikwenda kokote katika pande nne walikoelekea wale makerubi. Magurudumu hayakugeuka wakati makerubi yalipokwenda. Makerubi walikwenda upande wowote kichwa kilikoelekea pasipo kugeuka walipokuwa wakienda. 12Miili yao yote, pamoja na migongo yao, mikono na mabawa yao yote yalikuwa yamejaa macho kabisa kama yalivyokuwa yale magurudumu yao manne. 13Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.” 14Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa kama vile wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai. 15Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.