Kutoka 8:13
Exodus 8:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye Bwana akafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani.
Exodus 8:13 in English
Exodus 8:13 · Berean Standard Bible
And the LORD did as Moses requested, and the frogs in the houses, the courtyards, and the fields died.
Context
11Vyura wataondoka kwako na katika nyumba zako, kwa maafisa wako na kwa watu wako, ila watabakia katika Mto Naili tu.” 12Baada ya Mose na Aroni kuondoka kwa Farao, Mose akamlilia Bwana kuhusu vyura aliokuwa amewaleta kwa Farao. 13Naye Bwana akafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani. 14Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. 15Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile Bwana alivyokuwa amesema.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.