Kutoka 4:3
Exodus 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akasema, “Itupe chini.” Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia.
Exodus 4:3 in English
Exodus 4:3 · Berean Standard Bible
“Throw it on the ground,” said the LORD. So Moses threw it on the ground, and it became a snake,* and he ran from it.
Context
1Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?” 2Ndipo Bwana akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”
Akajibu, “Fimbo.” 3Bwana akasema, “Itupe chini.”
Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4Kisha Bwana akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 5Bwana akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.