Kutoka 39:42
Exodus 39:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose.
Exodus 39:42 in English
Exodus 39:42 · Berean Standard Bible
The Israelites had done all the work just as the LORD had commanded Moses.
Context
40mapazia ya ua pamoja na nguzo na vitako vyake, pia na pazia kwa ajili ya ingilio la kwenye ua; kamba zake na vigingi vya hema kwa ajili ya ua; vyombo vyote vilivyohitajiwa kwa ajili ya maskani, Hema la Kukutania; 41na mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani. 42Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Bwana alivyokuwa amemwagiza Mose. 43Mose akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Mose akawabariki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.