Native Bible

Exodus 36:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,* na upana wa dhiraa nne*

Exodus 36:9 in English

Exodus 36:9 · Berean Standard Bible

Each curtain was twenty-eight cubits long and four cubits wide;* all the curtains were the same size.

Context

7kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote. 8Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. 9Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,* na upana wa dhiraa nne* 10Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 11Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.