Kutoka 32:3
Exodus 32:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni.
Exodus 32:3 in English
Exodus 32:3 · Berean Standard Bible
Then all the people took off their gold earrings and brought them to Aaron.
Context
1Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.” 2Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” 3Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni. 4Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.” 5Aroni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa Bwana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.