Kutoka 32:16
Exodus 32:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao.
Exodus 32:16 in English
Exodus 32:16 · Berean Standard Bible
The tablets were the work of God, and the writing was the writing of God, engraved on the tablets.
Context
14Kisha Bwana akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia. 15Mose akageuka, akashuka kutoka mlimani akiwa na vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake. Vilikuwa vimeandikwa pande zote mbili, mbele na nyuma. 16Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao. 17Yoshua aliposikia sauti za watu wakipiga kelele, akamwambia Mose, “Kuna sauti ya vita kambini.” 18Mose akajibu:
“Si sauti ya ushindi,
wala si sauti ya kushindwa;
ni sauti ya kuimba ninayosikia.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.