Native Bible

Exodus 29:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake.

Exodus 29:15 in English

Exodus 29:15 · Berean Standard Bible

Take one of the rams, and Aaron and his sons shall lay their hands on its head.

Context

13Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu. 14Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi. 15“Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. 16Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyize pande zote za hayo madhabahu. 17Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.