Native Bible

Exodus 26:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,* na upana wa dhiraa nne.

Exodus 26:8 in English

Exodus 26:8 · Berean Standard Bible

Each of the eleven curtains is to be the same size—thirty cubits long and four cubits wide.*

Context

6Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja. 7“Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 8Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,* na upana wa dhiraa nne. 9Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya maskani. 10Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.