Kutoka 17:1
Exodus 17:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Bwana alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
Exodus 17:1 in English
Exodus 17:1 · Berean Standard Bible
Then the whole congregation of Israel left the Desert of Sin,* moving from place to place as the LORD commanded. They camped at Rephidim, but there was no water for the people to drink.
Context
1Jumuiya yote ya Israeli ikaondoka kutoka Jangwa la Sini, ikisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Bwana alivyoagiza. Wakapiga kambi huko Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa. 2Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.”
Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Bwana?” 3Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanungʼunika dhidi ya Mose, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.