Kutoka 16:30
Exodus 16:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba.
Exodus 16:30 in English
Exodus 16:30 · Berean Standard Bible
So the people rested on the seventh day.
Context
28Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini? 29Fahamuni kuwa Bwana amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” 30Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba. 31Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana* Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. 32Mose akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.