Native Bible

Exodus 15:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”

Exodus 15:24 in English

Exodus 15:24 · Berean Standard Bible

So the people grumbled against Moses, saying, “What are we to drink?”

Context

22Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. 23Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara*) 24Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?” 25Ndipo Mose akamlilia Bwana, naye Bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu. Huko Bwana akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. 26Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.