Kutoka 12:26
Exodus 12:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’
Exodus 12:26 in English
Exodus 12:26 · Berean Standard Bible
When your children ask you, ‘What does this service mean to you?’
Context
24“Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. 25Mtakapoingia katika nchi Bwana atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. 26Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ 27Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Bwana, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu. 28Waisraeli wakafanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.