Esta 9:11
Esther 9:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.
Esther 9:11 in English
Esther 9:11 · Berean Standard Bible
On that day the number of those killed in the citadel of Susa was reported to the king,
Context
9Parmashta, Arisai, Aridai na Waizatha, 10wana kumi wa Hamani mwana wa Hamedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchukua nyara. 11Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani. 12Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.” 13Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.