Mhubiri 2:18
Ecclesiastes 2:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu.
Ecclesiastes 2:18 in English
Ecclesiastes 2:18 · Berean Standard Bible
I hated all for which I had toiled under the sun, because I must leave it to the man who comes after me.
Context
16Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,
kama ilivyo kwa mpumbavu,
hatakumbukwa kwa muda mrefu,
katika siku zijazo wote watasahaulika.
Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,
mtu mwenye hekima pia lazima atakufa! 17Kwa hiyo nikachukia maisha, kwa sababu kazi inayofanyika chini ya jua ilikuwa masikitiko kwangu. Yote hayo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 18Nikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu. 19Nani ajuaye kama atakuwa ni mtu mwenye hekima au mpumbavu? Lakini hata hivyo yeye ndiye atakayetawala kazi zote ambazo nimemiminia juhudi na ustadi chini ya jua. Hili nalo ni ubatili. 20Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi yangu yote niliyoifanya kwa taabu chini ya jua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.