Native Bible

Deuteronomy 4:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.

Deuteronomy 4:24 in English

Deuteronomy 4:24 · Berean Standard Bible

For the LORD your God is a consuming fire,* a jealous God.

Context

22Nitakufa katika nchi hii; sitavuka Yordani, lakini ninyi ni karibu mvuke mkaimiliki ile nchi nzuri. 23Jihadharini msilisahau Agano la Bwana Mungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho Bwana Mungu wenu amewakataza. 24Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu. 25Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wenu na kumfanya awe na hasira, 26ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.