Kumbukumbu 24:17
Deuteronomy 24:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani.
Deuteronomy 24:17 in English
Deuteronomy 24:17 · Berean Standard Bible
Do not deny justice to the foreigner or the fatherless, and do not take a widow’s cloak as security.
Context
15Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi. 16Baba wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe. 17Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani. 18Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa huko Misri, naye Bwana Mungu wenu akawakomboa kutoka huko. Hii ndiyo sababu ninawaamuru kutenda hili. 19Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Bwana Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.