Kumbukumbu 24:11
Deuteronomy 24:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ukae nje na umwache huyo mtu uliyemkopesha akuletee hiyo rehani.
Deuteronomy 24:11 in English
Deuteronomy 24:11 · Berean Standard Bible
You are to stand outside while the man to whom you are lending brings the security out to you.
Context
9Kumbukeni kile Bwana Mungu wenu alichomfanyia Miriamu njiani baada ya ninyi kutoka Misri. 10Unapomkopesha jirani yako chochote, usiingie nyumbani kwake kutwaa kile anachokitoa kama rehani. 11Ukae nje na umwache huyo mtu uliyemkopesha akuletee hiyo rehani. 12Ikiwa mtu huyo ni maskini, usiende kulala ukiwa na hiyo rehani yake katika milki yako. 13Rudisha vazi lake kabla ya machweo ya jua ili apate kulilalia. Kisha atakushukuru na kitaonekana kama kitendo cha haki mbele za Bwana Mungu wako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.