Native Bible

Deuteronomy 21:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake.

Deuteronomy 21:19 in English

Deuteronomy 21:19 · Berean Standard Bible

his father and mother are to lay hold of him and bring him to the elders of his city, to the gate of his hometown,

Context

17Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyo navyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye. 18Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi, 19baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake. 20Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.” 21Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.