Kumbukumbu 15:13
Deuteronomy 15:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu.
Deuteronomy 15:13 in English
Deuteronomy 15:13 · Berean Standard Bible
And when you release him, do not send him away empty-handed.
Context
11Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu. 12Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru. 13Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu. 14Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo Bwana Mungu wako alivyokubariki. 15Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri naye Bwana Mungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.