Native Bible

Deuteronomy 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe,

Deuteronomy 12:8 in English

Deuteronomy 12:8 · Berean Standard Bible

You are not to do as we are doing here today, where everyone does what seems right in his own eyes.

Context

6hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ngʼombe pamoja na mbuzi na kondoo. 7Hapo, katika uwepo wa Bwana Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mungu wenu amewabariki. 8Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe, 9kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mungu wenu anawapa. 10Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.