Native Bible

Daniel 9:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu.

Daniel 9:22 in English

Daniel 9:22 · Berean Standard Bible

He instructed me and spoke with me, saying: “O Daniel, I have come now to give you insight and understanding.

Context

20Basi, nilipokuwa bado nikinena na kuomba, nikiungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na nikifanya maombi yangu kwa Bwana Mungu wangu kwa ajili ya mlima wake mtakatifu, 21wakati nilipokuwa bado katika maombi, Gabrieli, yule mtu niliyekuwa nimemwona katika maono hapo awali, alinijia kwa kasi karibu wakati wa kutoa dhabihu ya jioni. 22Akanielimisha na kuniambia, “Danieli, sasa nimekuja kukupa akili na ufahamu. 23Mara ulipoanza kuomba, jibu lilitolewa, ambalo nimekuja kukupasha habari, kwa maana wewe unapendwa sana. Kwa hiyo, tafakari ujumbe huu na uelewe maono haya: 24“Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na kwa ajili ya mji wako mtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, kuleta haki ya milele, kutia muhuri maono na unabii, na pia kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu sana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.