Danieli 6:25
Daniel 6:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana!
Daniel 6:25 in English
Daniel 6:25 · Berean Standard Bible
Then King Darius wrote to the people of every nation and language throughout the land: “May your prosperity abound.
Context
23Mfalme akafurahi mno, naye akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake. 24Kwa amri ya mfalme, wale watu waliokuwa wamemshtaki Danieli kwa uongo waliletwa na kutupwa ndani ya lile tundu la simba, pamoja na wake zao na watoto wao. Nao kabla hawajafika chini kwenye sakafu ya lile tundu, simba wakawakamata na kusaga mifupa yao yote. 25Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote:
“Ninyi na mstawi sana! 26“Natoa amri hii, kwamba katika kila sehemu ya ufalme wangu, lazima watu wamwogope na kumheshimu Mungu wa Danieli.
“Kwa maana yeye ni Mungu aliye hai,
naye hudumu milele,
ufalme wake hautaangamizwa,
nao utawala wake hauna mwisho. 27Huponya na kuokoa;
hufanya ishara na maajabu
mbinguni na duniani.
Amemwokoa Danieli
kutoka nguvu za simba.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.