Native Bible

Daniel 3:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini,* na upana wa dhiraa sita,* akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli.

Daniel 3:1 in English

Daniel 3:1 · Berean Standard Bible

King Nebuchadnezzar made a golden statue * sixty cubits high and six cubits wide,* and he set it up on the plain of Dura in the province of Babylon.

Context

1Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu, yenye kimo cha dhiraa sitini,* na upana wa dhiraa sita,* akaisimamisha kwenye tambarare ya Dura katika jimbo la nchi ya Babeli. 2Kisha mfalme akaita wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wote wa jimbo kuja kuizindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. 3Basi wakuu, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, waamuzi, mahakimu na maafisa wengine wa jimbo walikusanyika ili kuizindua sanamu ile Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha, nao wakasimama mbele ya hiyo sanamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.