Danieli 11:34
Daniel 11:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watakapoanguka, watapokea msaada kidogo, nao wengi ambao si waaminifu wataungana nao.
Daniel 11:34 in English
Daniel 11:34 · Berean Standard Bible
Now when they fall, they will be granted a little help, but many will join them insincerely.
Context
32Kwa udanganyifu atapotosha wale walionajisi agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti. 33“Wenye hekima watawafundisha wengi, ingawa kwa kitambo watauawa kwa upanga au kuchomwa moto, au kukamatwa au kufanywa mateka. 34Watakapoanguka, watapokea msaada kidogo, nao wengi ambao si waaminifu wataungana nao. 35Baadhi ya wenye hekima watajikwaa, ili waweze kusafishwa, kutakaswa na kufanywa wasio na waa mpaka wakati wa mwisho, kwa maana bado litakuja kwa wakati ulioamriwa. 36“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.