Amosi 7:3
Amos 7:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo Bwana akaghairi. Kisha Bwana akasema, “Hili halitatokea.”
Amos 7:3 in English
Amos 7:3 · Berean Standard Bible
So the LORD relented from this plan. “It will not happen,” He said.
Context
1Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. 2Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” 3Kwa hiyo Bwana akaghairi.
Kisha Bwana akasema, “Hili halitatokea.” 4Hili ndilo Bwana Mwenyezi alilonionyesha katika maono: Bwana Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. 5Ndipo nikalia, “Bwana Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.