Native Bible

Acts 9:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi wakafanya shauri kumuua Sauli.

Acts 9:23 in English

Acts 9:23 · Berean Standard Bible

After many days had passed, the Jews conspired to kill him,

Context

21Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa na kuuliza, “Huyu si yule mtu aliyesababisha maangamizi makuu huko Yerusalemu miongoni mwa watu waliolitaja jina hili? Naye si amekuja hapa kwa kusudi la kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wafungwa mbele ya viongozi wa makuhani?” 22Sauli akazidi kuwa hodari na kuwashangaza Wayahudi walioishi Dameski kwa kuthibitisha kuwa Yesu ndiye Kristo.* 23Baada ya siku nyingi kupita, Wayahudi wakafanya shauri kumuua Sauli. 24Lakini shauri lao likajulikana kwa Sauli. Wayahudi wakawa wanalinda malango yote ya mji, usiku na mchana ili wapate kumuua. 25Lakini wafuasi wake wakamchukua usiku wakamshusha akiwa ndani ya kapu kupitia mahali penye nafasi ukutani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.