Native Bible

Acts 4:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakawaamuru watoke nje ya Baraza la Wayahudi* wakati wakisemezana jambo hilo wao kwa wao.

Acts 4:15 in English

Acts 4:15 · Berean Standard Bible

So they ordered them to leave the Sanhedrin * and then conferred together.

Context

13Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kujua ya kuwa walikuwa watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa sana, wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu. 14Lakini kwa kuwa walikuwa wanamwona yule kiwete aliyeponywa amesimama pale pamoja nao, hawakuweza kusema lolote kuwapinga. 15Wakawaamuru watoke nje ya Baraza la Wayahudi* wakati wakisemezana jambo hilo wao kwa wao. 16Wakaulizana, “Tuwafanyie nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. 17Lakini ili kuzuia jambo hili lisiendelee kuenea zaidi kwa watu, ni lazima tuwaonye watu hawa ili wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina la Yesu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.