Native Bible

Acts 23:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Askari walipofika Kaisaria, walimpa mtawala ile barua, na kumkabidhi Paulo kwake.

Acts 23:33 in English

Acts 23:33 · Berean Standard Bible

When the horsemen arrived in Caesarea, they delivered the letter to the governor and presented Paul to him.

Context

31Hivyo askari, kwa kufuata maelekezo waliyopewa, wakamchukua Paulo wakati wa usiku na kumleta mpaka Antipatri. 32Kesho yake wakawaacha wale wapanda farasi waendelee na safari wakiwa na Paulo, wao wakarudi kwenye ngome ya askari. 33Askari walipofika Kaisaria, walimpa mtawala ile barua, na kumkabidhi Paulo kwake. 34Mtawala alipokwisha kuisoma ile barua alimuuliza Paulo alikuwa mtu wa jimbo gani. Alipojua kuwa anatoka Kilikia, 35alisema, “Nitasikiliza shauri lako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.