Native Bible

Acts 20:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.

Acts 20:27 in English

Acts 20:27 · Berean Standard Bible

For I did not shrink back from declaring to you the whole will of God.

Context

25“Nami sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu ambaye nimemhubiria Ufalme wa Mungu katika kwenda kwangu huku na huko, atakayeniona uso tena. 26Kwa hiyo nawatangazia leo, sina hatia ya damu ya mtu awaye yote. 27Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu. 28Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. 29Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.