Native Bible

Acts 17:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi.

Acts 17:1 in English

Acts 17:1 · Berean Standard Bible

When they had passed through Amphipolis and Apollonia, they came to Thessalonica, where there was a Jewish synagogue.

Context

1Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. 2Kama desturi yake, Paulo aliingia ndani ya sinagogi, na kwa muda wa Sabato tatu akawa anahojiana nao kutoka kwenye Maandiko, 3akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Kristo* ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake, ndiye Kristo.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.