Native Bible

Acts 13:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao.

Acts 13:3 in English

Acts 13:3 · Berean Standard Bible

And after they had fasted and prayed, they laid their hands on them and sent them off.

Context

1Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. 2Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.” 3Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao. 4Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro. 5Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.