Native Bible

2 Timothy 3:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli.

2 Timothy 3:7 in English

2 Timothy 3:7 · Berean Standard Bible

who are always learning but never able to come to a knowledge of the truth.

Context

5wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu wa namna hiyo. 6Miongoni mwao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu na kuwachukua mateka wanawake wajinga, waliolemewa na dhambi zao na kuyumbishwa na aina zote za tamaa mbaya. 7Wakijifunza siku zote lakini kamwe wasiweze kufikia ujuzi wa kweli. 8Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Mose, vivyo hivyo watu hawa hupingana na ile kweli. Hawa ni watu wenye akili zilizopotoka, ambao wamekataliwa kwa mambo ya imani. 9Lakini hawataendelea sana, kwa sababu upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri upumbavu wa hao watu wawili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.