Native Bible

2 Thessalonians 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya?

2 Thessalonians 2:5 in English

2 Thessalonians 2:5 · Berean Standard Bible

Do you not remember that I told you these things while I was still with you?

Context

3Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. 4Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu. 5Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? 6Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. 7Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.