2 Samweli 3:35
2 Samuel 3:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!”
2 Samuel 3:35 in English
2 Samuel 3:35 · Berean Standard Bible
Then all the people came and urged David to eat something while it was still day, but David took an oath, saying, “May God punish me, and ever so severely, if I taste bread or anything else before the sun sets!”
Context
33Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri:
“Je, ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu? 34Mikono yako haikufungwa,
miguu yako haikufungwa pingu.
Ulianguka kama yeye aangukaye
mbele ya watu waovu.”
Nao watu wote wakamlilia tena. 35Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!” 36Watu wote wakaona hilo nao ikawapendeza; naam, kila kitu mfalme alichofanya kiliwapendeza. 37Kwa hiyo siku ile watu wote na Israeli yote wakajua kwamba mfalme hakushiriki katika mauaji ya Abneri mwana wa Neri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.