2 Samweli 16:20
2 Samuel 16:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako. Tufanye nini?”
2 Samuel 16:20 in English
2 Samuel 16:20 · Berean Standard Bible
Then Absalom said to Ahithophel, “Give me counsel. What should we do?”
Context
18Hushai akamwambia Absalomu, “La hasha, yeye aliyechaguliwa na Bwana, aliyechaguliwa na watu hawa, atakayechaguliwa tena na watu wote wa Israeli, huyu ndiye nitakayekuwa wake, nami nitabakia pamoja naye. 19Zaidi ya hayo, nimtumikie nani? Je, nisimtumikie mwana? Kama vile nilivyomtumikia baba yako, ndivyo nitakavyokutumikia wewe.” 20Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako. Tufanye nini?” 21Ahithofeli akamjibu, “Kutana kimwili na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza jumba la kifalme. Ndipo Israeli yote itakaposikia kwamba umejifanya chukizo kwa baba yako, nayo mikono ya kila mmoja aliye pamoja nawe itatiwa nguvu.” 22Kwa hiyo wakasimika hema kwa ajili ya Absalomu juu ya paa, naye akakutana kimwili na masuria wa baba yake mbele ya Israeli wote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.